| Chapter 1 |
1 |
Mimi Yakobo, mtumishi wa Mungu na wa Bwana Yesu Kristo, nawaandikia ninyi, makabila kumi na mawili, yaliyotawanyika ulimwenguni! Salaam! --
|
2 |
Ndugu zangu, muwe na furaha mnapopatwa na majaribu mbalimbali, --
|
3 |
kwani mwajua kwamba imani yenu ikisha stahimili, itawapatieni uvumilivu. --
|
4 |
Muwe na hakika kwamba uvumilivu wenu utawategemeza mpaka mwisho, mpate kuwa wakamilifu na watimilifu, bila kupungukiwa chochote. --
|
5 |
Lakini kama mmoja wenu ametindikiwa hekima, basi, anapaswa kumwomba Mungu ambaye atampatia; kwani Mungu huwapa wote kwa wingi na kwa ukarimu. --
|
6 |
Lakini anapaswa kuomba kwa imani bila mashaka yoyote. Mtu aliye na mashaka ni kama mawimbi ya bahari ambayo husukumwa na kutupwatupwa na upepo. --
|
7 |
Mtu wa namna hiyo, mwenye nia mbili na asiye na msimamo katika mwenendo wake wote, asidhani ya kwamba atapata chochote kile kutoka kwa Bwana. --
|
8 |
[] --
|
9 |
Ndugu aliye maskini anapaswa kufurahi wakati Mungu anapomkweza, --
|
10 |
naye tajiri anapaswa kufurahi anaposhushwa na Mungu. Maana tajiri atatoweka kama ua la porini. --
|
11 |
Jua huchomoza na kwa joto lake kali hukausha mimea, nayo maua yake huanguka, na uzuri wake wote huharibika. Vivyo hivyo, tajiri ataangamizwa katika shughuli zake. --
|
12 |
Heri mtu anayebaki mwaminifu katika majaribu, kwani akisha stahimili atapewa tuzo la uzima ambalo Mungu aliwaahidia wale wanaompenda. --
|
13 |
Kama mtu akijaribiwa, asiseme: "Ninajaribiwa na Mungu." Maana Mungu hawezi kujaribiwa na uovu, wala yeye hamjaribu mtu yeyote. --
|
14 |
Lakini mtu hujaribiwa anapovutwa na kunaswa na tamaa zake mbaya. --
|
15 |
Tamaa ikiiva huzaa dhambi; nayo dhambi ikikomaa huzaa kifo. --
|
16 |
Ndugu zangu wapenzi, msidanganyike! --
|
17 |
Kila kipaji chema na kila zawadi kamilifu hutoka mbinguni; hutoka kwa Baba, Muumba wa mianga, ambaye habadiliki wala hana alama yoyote ya ugeugeu. --
|
18 |
Kwa kupenda kwake mwenyewe alituzaa kwa neno lake la ukweli, ili tuwe namna ya matunda ya kwanza miongoni mwa viumbe vyake. --
|
19 |
Ndugu zangu wapenzi, kumbukeni jambo hili! Kila mtu na awe mwepesi wa kusikia lakini asiwe mwepesi wa kusema wala mwepesi wa kukasirika. --
|
20 |
Mwenye hasira hawezi kutimiza matakwa ya Mungu yaliyo ya haki. --
|
21 |
Kwa hiyo, tupilieni mbali mwenendo mchafu na tabia zote mbovu; jiwekeni chini ya Mungu na kupokea ule ujumbe uliopandwa mioyoni mwenu, ambao waweza kuziokoa nafsi zenu. --
|
22 |
Msijidanganye wenyewe kwa kusikiliza tu neno lake, bali litekelezeni kwa vitendo. --
|
23 |
Yeyote anayesikiliza hilo neno lakini halitekelezi, huyo ni kama mtu anayejiangalia sura yake mwenyewe katika kioo. --
|
24 |
Hujiangalia mwenyewe, kisha huenda zake, na mara husahau jinsi alivyo. --
|
25 |
Lakini mtu anayeangalia kwa makini sheria kamilifu ambayo huwapa watu uhuru, mtu anayeendelea kuizingatia, na si kuisikia tu na kuisahau baadaye, bali anaitekeleza, mtu huyo atabarikiwa katika kila kitu anachofanya. --
|
26 |
Kama mtu akijiona kuwa ni mtu mwenye dini, lakini hawezi kuutawala ulimi wake, dini yake haifai kitu, na anajidanganya mwenyewe. --
|
27 |
Dini iliyo safi na isiyo na hitilafu mbele ya Mungu Baba ni hii: Kuwasaidia yatima na wajane katika shida zao, na kujilinda mwenyewe usichafuliwe na ulimwengu huu. --
|