| Chapter 17 |
1 |
Kisha, Yesu akawaambia wanafunzi wake, "Haiwezekani kabisa kusitokee vikwazo vinavyosababisha dhambi; lakini ole wake mtu yule atakayevisababisha. --
|
2 |
Ingekuwa afadhali kwake kufungiwa shingoni jiwe kubwa la kusagia na kutoswa baharini, kuliko kumkwaza mmoja wa wadogo hawa. --
|
3 |
Jihadharini! Kama ndugu yako akikukosea, mwonye; akitubu, msamehe. --
|
4 |
Na kama akikukosea mara saba kwa siku, na kila mara akarudi kwako akisema `Nimetubu`, lazima umsamehe." --
|
5 |
Mitume wakamwambia Bwana, "Utuongezee imani." --
|
6 |
Naye Bwana akajibu, "Kama imani yenu ingekuwa ndogo hata kama chembe ndogo ya haradali, mngeweza kuuambia mti huu wa mkuyu: `Ng`oka ukajipandikize baharini`, nao ungewatii. --
|
7 |
"Tuseme mmoja wenu ana mtumishi ambaye analima shambani au anachunga kondoo. Je, anaporudi kutoka shambani, atamwambia: `Haraka, njoo ule chakula?` --
|
8 |
La! Atamwambia: `Nitayarishie chakula, ujifunge tayari kunitumikia mpaka nitakapomaliza kula na kunywa, ndipo nawe ule na unywe.` --
|
9 |
Je utamshukuru huyo mtumishi kwa sababu ametimiza aliyoamriwa? --
|
10 |
Hali kadhalika na ninyi mkisha fanya yote mliyoamriwa, semeni: `Sisi ni watumishi tusio na faida, tumetimiza tu yale tuliyotakiwa kufanya."` --
|
11 |
Yesu akiwa safarini kwenda Yerusalemu alipitia mipakani mwa Samaria na Galilaya. --
|
12 |
Alipokuwa anaingia katika kijiji kimoja, watu kumi wenye ukoma walikutana naye, wakasimama kwa mbali. --
|
13 |
Wakapaza sauti wakisema, "Yesu Mwalimu, tuonee huruma!" --
|
14 |
Alipowaona akawaambia, "Nendeni mkajionyeshe kwa makuhani." Basi, ikawa walipokuwa wanakwenda, wakatakasika. --
|
15 |
Mmoja wao alipoona kwamba ameponywa alirudi akimtukuza Mungu kwa sauti kubwa. --
|
16 |
Akajitupa chini mbele ya miguu ya Yesu huku akimshukuru. Huyo alikuwa Msamaria. --
|
17 |
Hapo Yesu akasema, "Je, si watu kumi walitakaswa? Wale tisa wako wapi? --
|
18 |
Hakupatikana mwingine aliyerudi kumtukuza Mungu ila tu huyu mgeni?" --
|
19 |
Halafu akamwambia huyo mtu, "Simama, uende zako; imani yako imekuponya." --
|
20 |
Wakati mmoja, Mafarisayo walimwuliza Yesu, "Ufalme wa Mungu utakuja lini?" Naye akawajibu, "Ufalme wa Mungu hauji kwa namna itakayoweza kuonekana. --
|
21 |
Wala hakuna atakayeweza kusema, `Uko hapa`, au `Uko pale`. Kwa kweli Ufalme wa Mungu uko kati yenu." --
|
22 |
Halafu akawaambia wanafunzi wake, "Siku zinakuja ambapo mtatamani kuona mojawapo ya siku za Mwana wa Mtu, lakini hamtaiona. --
|
23 |
Na watu watawaambieni: `Tazameni yuko hapa`; ninyi msitoke wala msiwafuate. --
|
24 |
Kwa maana kama vile umeme unavyotokea ghafla na kuangaza anga upande mmoja hadi mwingine, ndivyo Mwana wa Mtu atakavyokuwa siku yake. --
|
25 |
Lakini kabla ya hayo, itambidi ateseke sana na kukataliwa na kizazi hiki. --
|
26 |
Kama ilivyokuwa nyakati za Noa, ndivyo itakavyokuwa katika siku za Mwana wa Mtu. --
|
27 |
Watu waliendelea kula na kunywa, kuoa na kuolewa mpaka wakati ule Noa alipoingia katika safina. Gharika ikatokea na kuwaangamiza wote. --
|
28 |
Itakuwa kama ilivyotokea wakati wa Loti. Watu waliendelea kula na kunywa, kununua na kuuza, kupanda mbegu na kujenga. --
|
29 |
Lakini siku ile Loti alipoondoka Sodoma, moto na kiberiti vikanyesha kama mvua kutoka mbinguni na kuwaangamiza wote. --
|
30 |
Ndivyo itakavyokuwa siku ile Mwana wa Mtu atakapofunuliwa. --
|
31 |
"Siku hiyo, yeyote atakayekuwa juu ya paa asishuke nyumbani kuchukua mali yake. Kadhalika, naye atakayekuwa shambani asirudi nyuma. --
|
32 |
Kumbukeni yaliyompata mke wa Loti. --
|
33 |
Yeyote anayetaka kuiokoa nafsi yake, ataipoteza; na yeyote anayeipoteza, ataiokoa. --
|
34 |
Nawaambieni, siku ile usiku watu wawili watakuwa wanalala pamoja, mmoja atachukuliwa na yule mwingine ataachwa. --
|
35 |
Wanawake wawili watakuwa wakisaga nafaka pamoja; mmoja atachukuliwa na mwingine ataachwa."*fc* atachukuliwa na mwingine ataachwa.\ie --
|
36 |
missing --
|
37 |
Hapo wakamwuliza, "Ni wapi Bwana?" Naye akawaambia, "Ulipo mzoga, ndipo tai watakapokusanyikia." --
|