| Chapter 1 |
1 |
Mheshimiwa Theofilo: Watu wengi wamejitahidi kuandika juu ya mambo yale yaliyotendeka kati yetu. --
|
2 |
Waliandika kama tulivyoelezwa na wale walioyaona kwa macho yao tangu mwanzo, na waliotangaza ujumbe huo. --
|
3 |
Inafaa nami pia, Mheshimiwa, baada ya kuchunguza kwa makini mambo yote tangu mwanzo, nikuandikie kwa mpango, --
|
4 |
ili nawe uweze kujionea mwenyewe ukweli wa mambo yale uliyofundishwa. --
|
5 |
Wakati Herode alipokuwa mfalme wa Yudea, kulikuwa na kuhani mmoja jina lake Zakaria, wa kikundi cha Abia. Mke wake alikuwa anaitwa Elisabeti, naye alikuwa wa ukoo wa kuhani Aroni. --
|
6 |
Wote wawili walikuwa wanyofu mbele ya Mungu, wakiishi kwa kufuata amri na maagizo yote ya Bwana bila lawama. --
|
7 |
Lakini hawakuwa wamejaliwa watoto kwa vile Elisabeti alikuwa tasa, nao wote wawili walikuwa wazee sana. --
|
8 |
Siku moja, ilipokuwa zamu yake ya kutoa huduma ya ukuhani mbele ya Mungu, --
|
9 |
Zakariya alichaguliwa kwa kura, kama ilivyokuwa desturi, kuingia hekaluni ili afukize ubani. --
|
10 |
Watu, umati mkubwa, walikuwa wamekusanyika nje wanasali wakati huo wa kufukiza ubani. --
|
11 |
Malaika wa Bwana akamtokea humo ndani, akasimama upande wa kulia wa madhabahu ya kufukizia ubani. --
|
12 |
Zakariya alipomwona alifadhaika, hofu ikamwingia. --
|
13 |
Lakini malaika akamwambia, "Zakariya, usiogope, kwa maana sala yako imesikilizwa, na Elisabeti mkeo atakuzalia mtoto wa kiume, nawe utampa jina Yohane. --
|
14 |
Utakuwa na furaha kubwa na watu wengi watashangilia kwa sababu ya kuzaliwa kwake. --
|
15 |
Atakuwa mkuu mbele ya Bwana. Hatakunywa divai wala kileo, atajazwa Roho Mtakatifu tangu tumboni mwa mama yake. --
|
16 |
Atawaelekeza wengi wa watu wa Israeli kwa Bwana Mungu wao. --
|
17 |
Atamtangulia Bwana akiongozwa na nguvu na roho kama Eliya. Atawapatanisha kina baba na watoto wao; atawafanya wasiotii wawe na fikira za uadilifu, na hivyo amtayarishie Bwana watu wake." --
|
18 |
Zakariya akamwambia huyo malaika, "Ni kitu gani kitakachonihakikishia jambo hilo? Mimi ni mzee, hali kadhalika na mke wangu." --
|
19 |
Malaika akamjibu, "Mimi ni Gabrieli, nisimamaye mbele ya Mungu, na nimetumwa niseme nawe, nikuletee hii habari njema. --
|
20 |
Sikiliza, utakuwa bubu kwa sababu huyasadiki haya maneno yatakayotimia kwa wakati wake. Hutaweza kusema mpaka hayo niliyokuambia yatakapotimia." --
|
21 |
Wakati huo, wale watu walikuwa wanamngoja Zakariya huku wakishangaa juu ya kukawia kwake Hekaluni. --
|
22 |
Alipotoka nje, hakuweza kusema nao. Ikawa dhahiri kwao kwamba alikuwa ameona maono Hekaluni. Lakini akawa anawapa ishara kwa mikono, akabaki bubu. --
|
23 |
Zamu yake ya kuhudumu ilipokwisha, alirudi nyumbani. --
|
24 |
Baadaye Elisabeti mkewe akapata mimba. Akajificha nyumbani kwa muda wa miezi mitano, akisema: --
|
25 |
"Hivi ndivyo alivyonitendea Bwana; ameniangalia na kuniondolea aibu niliyokuwa nayo mbele ya watu." --
|
26 |
Mnamo mwezi wa sita, malaika Gabrieli alitumwa na Mungu aende kwenye mji uitwao Nazareti huko Galilaya, --
|
27 |
kwa msichana mmoja aitwaye Maria, mchumba wa mtu mmoja jina lake Yosefu, wa ukoo wa Daudi. --
|
28 |
Malaika akamwendea, akamwambia, "Salamu Maria! Umejaliwa neema nyingi! Bwana yu pamoja nawe." --
|
29 |
Maria aliposikia maneno hayo alifadhaika sana, akawaza: maneno haya yanamaanisha nini? --
|
30 |
Malaika akamwambia, "Usiogope Maria, kwa maana Mungu amekujalia neema. --
|
31 |
Utachukua mimba, utamzaa mtoto wa kiume na utampa jina Yesu. --
|
32 |
Yeye atakuwa mkuu na ataitwa Mwana wa Mungu Mkuu. Bwana Mungu atampa kiti cha mfalme Daudi, babu yake. --
|
33 |
Kwa hivyo atautawala ukoo wa Yakobo milele, na ufalme wake hautakuwa na mwisho." --
|
34 |
Maria akamjibu, "Yatawezekanaje hayo, hali mimi ni bikira?" --
|
35 |
Malaika akamjibu, "Roho Mtakatifu atakushukia, na uwezo wake Mungu Mkuu utakujia kama kivuli; kwa sababu hiyo, mtoto atakayezaliwa ataitwa Mtakatifu, Mwana wa Mungu. --
|
36 |
Ujue pia kwamba hata Elisabeti, jamaa yako, naye amepata mimba ingawa ni mzee, na sasa ni mwezi wa sita kwake yeye ambaye watu walimfahamu kuwa tasa. --
|
37 |
Kwa maana hakuna jambo lisilowezekana kwa Mungu." --
|
38 |
Maria akasema, "Mimi ni mtumishi wa Bwana, nitendewe kama ulivyosema." Kisha yule malaika akaenda zake. --
|
39 |
Siku kadhaa baadaye, Maria alifunga safari akaenda kwa haraka hadi mji mmoja ulioko katika milima ya Yuda. --
|
40 |
Huko, aliingia katika nyumba ya Zakariya, akamsalimu Elisabeti. --
|
41 |
Mara tu Elisabeti aliposikia sauti ya Maria, mtoto mchanga tumboni mwake Elisabeti akaruka. Naye Elisabeti akajazwa Roho Mtakatifiu, --
|
42 |
akasema kwa sauti kubwa, "Umebarikiwa kuliko wanawake wote, naye utakayemzaa amebarikiwa. --
|
43 |
Mimi ni nani hata mama wa Bwana wangu afike kwangu? --
|
44 |
Nakwambia, mara tu niliposikia sauti yako, mtoto mchanga tumboni mwangu aliruka kwa furaha. --
|
45 |
Heri yako wewe uliyesadiki kwamba yatatimia yale Bwana aliyokwambia." --
|
46 |
Naye Maria akasema, --
|
47 |
"Moyo wangu wamtukuza Bwana, roho yangu inafurahi kwa sababu ya Mungu Mwokozi wangu. --
|
48 |
Kwa kuwa amemwangalia kwa huruma mtumishi wake mnyenyekevu. Hivyo tangu sasa watu wote wataniita mwenye heri. --
|
49 |
Kwa kuwa Mwenyezi Mungu amenitendea makuu, jina lake ni takatifu. --
|
50 |
Huruma yake kwa watu wanaomcha hudumu kizazi hata kizazi. --
|
51 |
Amefanya mambo makuu kwa mkono wake: amewatawanya wenye kiburi katika mawazo ya mioyo yao; --
|
52 |
amewashusha wenye nguvu kutoka vitu vyao vya enzi, akawakweza wanyenyekevu. --
|
53 |
Wenye njaa amewashibisha mema, matajiri amewaacha waende mikono mitupu. --
|
54 |
Amemsaidia Israeli mtumishi wake, akikumbuka huruma yake. --
|
55 |
Kama alivyowaahidia wazee wetu Abrahamu na wazawa wake hata milele." --
|
56 |
Maria alikaa na Elisabeti kwa muda upatao miezi mitatu, halafu akarudi nyumbani kwake. --
|
57 |
Wakati wa kujifungua kwake Elisabeti ulifika, akajifungua mtoto wa kiume. --
|
58 |
Jirani na watu wa jamaa yake walipopata habari kwamba Bwana amemwonea huruma kubwa, walifurahi pamoja naye. --
|
59 |
Halafu siku ya nane walifika kumtahiri mtoto, wakataka kumpa jina la baba yake, Zakariya. --
|
60 |
Lakini mama yake akasema, "La, sivyo, bali ataitwa Yohane." --
|
61 |
Wakamwambia, "Mbona hakuna yeyote katika ukoo wake mwenye jina hilo?" --
|
62 |
Basi, wakamwashiria baba yake wapate kujua alitaka mtoto wake apewe jina gani. --
|
63 |
Naye akaomba kibao cha kuandikia, akaandika hivi: "Yohane ndilo jina lake." Wote wakastaajabu. --
|
64 |
Papo hapo midomo na ulimi wake Zakariya vikafunguliwa, akawa anaongea akimsifu Mungu. --
|
65 |
Hofu ikawaingia jirani wote, na habari hizo zikaenea kila mahali katika milima ya Yudea. --
|
66 |
Wote waliosikia mambo hayo waliyatafakari mioyoni mwao wakisema: "Mtoto huyu atakuwa mtu wa namna gani?" Maana, hakika nguvu ya Bwana ilikuwa pamoja naye. --
|
67 |
Zakariya, baba yake mtoto, akajazwa Roho Mtakatifu, akatamka ujumbe wa Mungu: --
|
68 |
"Asifiwe Bwana Mungu wa Israeli, kwani amekuja kuwasaidia na kuwakomboa watu wake. --
|
69 |
Ametupatia Mwokozi shujaa, mzawa wa Daudi mtumishi wake. --
|
70 |
Aliahidi hapo kale kwa njia ya manabii wake watakatifu, --
|
71 |
kwamba atatuokoa mikononi mwa adui zetu na kutoka mikononi mwa wote wanaotuchukia. --
|
72 |
Alisema atawahurumia wazee wetu, na kukumbuka agano lake takatifu. --
|
73 |
Kiapo alichomwapia Abrahamu baba yetu, ni kwamba atatujalia sisi --
|
74 |
tukombolewe kutoka adui zetu, tupate kumtumikia bila hofu, --
|
75 |
kwa unyofu na uadilifu mbele yake, siku zote za maisha yetu. --
|
76 |
Nawe mwanangu, utaitwa, nabii wa Mungu Mkuu, utamtangulia Bwana kumtayarishia njia yake; --
|
77 |
kuwatangazia watu kwamba wataokolewa kwa kuondolewa dhambi zao. --
|
78 |
Mungu wetu ni mpole na mwenye huruma. Atasababisha pambazuko angavu la ukombozi litujie kutoka juu, --
|
79 |
na kuwaangazia wote wanaokaa katika giza kuu la kifo, aongoze hatua zetu katika njia ya amani." --
|
80 |
Mtoto akakua, akapata nguvu rohoni. Alikaa jangwani mpaka alipojionyesha rasmi kwa watu wa Israeli. --
|